MWANAFUNZI AKUTWA AMEKUFA KATIKA CHUMBA CHA "BOYFRIEND WAKE" BAADA YA JARIBIO LA KUTOA MIMBA KUSHINDIKANA


Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Iringa aliyetambuliwa kwa jina la Yasinta Kasuga amekutwa amekufa eneo la Ngome katika Manispaa ya Iringa akiwa ndani ya chumba cha kijana ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini mjini Iringa.

Taarifa za mashuhuda wa tukio hilo ambao wameteta na mtandao huu  wamedai kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akifika katika nyumba ya mwanafunzi huyo mara kwa mara na wamekuwa wakiishi kama mke na mume japo wote ni wanafunzi.

Shuhuda hao walisema kuwa kutokana na mazoea hayo walichukulia watu hao kama ni wapenzi na kuwa hata siku ya tukio walipotapa taarifa ya mwanafunzi huyo kufa walitegemea kijana huyo angewajulisha.

Cha kushangaza kijana huyo hakupata kuonekana kabisa na badala yake aliutelekeza mwili wa mwanafunzi huyo katika chumba chake.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla (pichani) limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa katika chumba hicho walikuta dripu na dawa nyingine ambazo zinaonyesha kuwa mwanafunzi huyo kifo chake kimetokana na kutaka kujaribu kutoa mimba.

Posted by Bigie on 2:22 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.