SALOME NDUMBAGWE ("THEA ") AMSHUTUMU "MONALISA" NA KUDAI KUWA NI MNAFIKI KWA KUWA ANAFUFUA BIFU LILILOISHA....
JAMII 6:48 PM
MSANII wa filamu Bongo, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ (pichani) amemtuhumu mwigizaji mwenzake, Yvone Cherry Ngatwika ‘Monalisa’ kuwa ni mnafiki kwani anafufua bifu lililoisha.
Akizungumza na Mpekuzi wetu jijini Dar, Thea alisema kuwa amefikia hatua ya kusema hivyo kufuatia mwenzake huyo kulitonya gazeti moja maarufu hapa nchini kwamba bifu lao la nyuma halijafutika.
Thea ambaye ni mke wa msanii, Michael Sangu ‘Mike’ alikiri kuwahi kutokea kwa bifu kati yao lakini akasema walishasuluhishwa na kumaliza tofauti hizo, lakini anashangaa kusikia Mona analiendeleza.
“Ni kweli tulikuwa na bifu la muda mrefu, lakini tuliitwa tukasuluhishwa yakaisha na kila mmoja akawa na heshima kwa mwenzake. Nashangaa hivi karibuni Monalisa anasema kuwa bifu hilo bado ni bichi, huu kwangu ni unafiki,” alisema Thea.