SCENE ZA MAHABA ZA "IRENE UWOYA" ZA MTESA MUMEWE NDIKUMANA


Vitendo vya ufuska kwa wasanii wa filamu Bongo wanapokuwa maeneo ya kurekodi (Location), vinadaiwa kumpa mateso makubwa mume wa Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’
 
Uchunguzi umebaini kuwa ni vigumu kwa baadhi ya wanaume kuvumilia wakiwaona wake zao wakifanyiwa vitendo vya kimahaba, hata kama wanaigiza.

Wapekuzi wetu kadhaa, wamekuwa wakiainisha namna wasanii wengi wa filamu walivyo wachafu huku baadhi yao wakikiri kufanya kweli wanaporekodi vipande (scene) vya mahaba ambapo wao huhama kwenye kuigiza na kufanya ngono kiukweli.

Lisemwalo lipo, kama halipo laja! Ili kujiridhisha na maneno hayo yaliyozagaa kitaani, hivi karibuni Ndikumana alitimba ‘lokesheni’ ambapo alishuhudia kwa macho yake mwenyewe bila miwani.


Katika filamu iliyoingia sokoni hivi karibuni ya Dj Ben, kwenye matukio ya nyuma ya pazia (behind the scene), Ndikumana anaonekana akimpiga chabo Uwoya akirekodi kipande kinachomuonesha akifanyiwa vitendo vya kimahaba live.

Wakati Ndikumana ambaye ni mwanasoka wa Rwanda akifanya hivyo, mpiga picha (cameraman) aliigeuzia upande aliokuwa jamaa huyo ambapo hakuna jinsi zaidi ya kujitahidi kuficha sura yake.


Ndoa ya wawili hao ilipopigwa kimbunga ikitaka kufutika, Ndikumana alimwambia mpekuzi wetu  kuwa alishamkataza Uwoya kucheza filamu za wasanii wenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Kanumba na Jacob Steven ‘JB’, lakini hakumsikia.

Alisema alijaribu kumwelewesha Uwoya kuwa afungue kampuni yake ya filamu kwani pamoja na yote, lakini hata fedha anazopata kupitia filamu za watu zinamtosha kwa ajili ya kununulia nguo tu kwa ajili ya filamu inayofuata.

Aliendelea kuweka kweupe kuwa alishamnunulia vifaa na kilichokuwa kimebaki ni kutafuta sehemu ya kuweka ofisi, lakini wakati hayo yakiendelea, mkewe alimgeuka na kurejea ulingoni kuigiza filamu za watu.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wanandoa hao waliojaliwa mtoto mmoja wa kiume, Krish, Ndikumana aliposhuhudia vitendo hivyo, ndipo alipobadilika na kukosa raha muda wote.

Ilielezwa kuwa hata kama Ndikumana hakumwambia Uwoya alivyojisikia, lakini akimsoma atagundua kuna kitu kinautesa moyo wake.


Ni katika kipindi hiki ambacho Ndikumana amekonda hivyo kutoa mwanya watu kudai kuwa kinachomtesa ni kile alichokutana nacho lokesheni.

Katika hilo, Ndikumana ana haya machache ya kusema : “Jamani please (tafadhali), niacheni nahitaji kupumzika na mambo hayo.”

Posted by Bigie on 1:33 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.