"MAVAZI YA "KICHANGUDOA" YAACHA GUMZO LA MWAKA KATIKA BIRTHDAY YA UWOYA
JAMII 12:53 AM
Miongoni mwa mambo yaliyoitingisha Bethidei ya msanii wa filamu Bongo, Irene Uwoya iliyofanyika hivi karibuni ni pamoja na vivazi vya kichangudoa walivyokuwa wamevaa baadhi ya mastaa.
Pati hiyo ilifanyika maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mastaa kibao baadhi wakiwa wamevalia vinguo hivyo vilivyoacha wazi sehemu nyeti za miili yao.
Aunti Ezekiel (pichani kushoto) , Husna Idd ‘Sajenti’, Kajala Masanja (pichani kulia) na Rachel Haule ni kati ya mademu waliokuwa wamevaa kihasara kiasi cha kuwafanya wasanii wenzao kuwachana.
“Dah! Hawa ndiyo wamevaa nini sasa? Matiti nje, mapaja nje, si bora wangekuja uchi kabisa? Huku ni kutuchoresha,” alisikika msanii mmoja kwa jazba
.
“Dah! Hawa ndiyo wamevaa nini sasa? Matiti nje, mapaja nje, si bora wangekuja uchi kabisa? Huku ni kutuchoresha,” alisikika msanii mmoja kwa jazba
.
Mwingine akadakia: “Kwa mavazi haya hatutaacha kuitwa malaya, utavaaje nguo hizi kama kweli unataka uheshimiwe?”
Licha ya baadhi ya watu waliokuwepo kwenye sherehe hiyo kuchukizwa na uvaaji wa mastaa hao, wenyewe walionekana kutojali na kufikia hatua ya kupozi kihasara zaidi na kuwapa wakati mgumu baadhi ya wanaume.