BABY MADAHA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI


Msanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya bongo Baby Madaha, yupo katika huzuni kubwa baada ya kumpoteza mama yake mazazi jana usiku baada ya kuumwa kwa muda mrefu. 

Mwili wa marehemu unasafirishwa leo kupelekwa Musoma nyumbani kwao ambapo mipango yote na taratibu za kuzika zitajulikana huko.

Mwandishi wa mtandao huu
alizungumza na Madaha ingawa hakuweza kuzungumza sana zaidi ya kutokwa machozi huku akisema kuwa amempoteza mama yake kipenzi ambaye alikuwa akimsapoti kwenye vitu vingi ndani ya maisha yake.

“Naumia sana lakini najua yote ni mipango ya Mungu kwani kila kitu kimepangwa, hivyo tunamuombea mama yetu aweze kwenda salama mbele za haki kwani sote hiyo ndiyo njia yetu,”
alisema kwa maskitiko makubwa sana.

Posted by Bigie on 3:42 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.