MITEGO YA KIMAPENZI YA AUNT LULU ILIGONGA UKUTA KWA KOFFI OLOMIDE


MTANGAZAJI mwenye matukio ya kumwaga Bongo, Lulu Mathias ‘Aunt Lulu’ alinaswa akihangaika kumtega mwanamuziki kutoka Kongo, Koffi ili aingie mkenge.

Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar wakati mwanamuziki huyo alipokuwa akifanya shoo yake.

“Lengo la Aunt Lulu aliyevaa vazi lililomuacha mgongo wake kujipitishapitisha back stage alipokuwa amekaa Koffi lilikuwa kumnasa msanii huyo lakini hadi anapanda jukwaani hakufanikiwa hata kuongea naye,” alisema mdau aliyemshuhudia.

Alipoulizwa kuhusu ishu hiyo , Aunt Lulu alifunguka:


“Wewe chezea mimi, mwenyewe alidata na mapigo yangu, sema ndiyo hivyo alikuwa bize na shoo, najuta kumkosa” alisema Aunt Lulu .

Posted by Bigie on 12:31 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.