Posted by Bigie
aunt lulu,
habari za kitaifa
1:34 AM
MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na mashoga pamoja na watoto.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo watakaojaa kwenye mazishi yake.
Alisema sababu kubwa ya msiba wake kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla hajabadili mfumo wa maisha anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku ya mazishi lazima wakumbuke fadhila.
“Unajua kufa ni kama kulala, naamini siku ya mazishi yangu watakaokuwa wengi ni watoto pamoja na mashoga ambao zamani nilikuwa mama yao, wengine ni waandishi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki,”alisema Aunty Lulu.
Posted by Bigie
aunt lulu,
habari za kitaifa
2:31 PM
MWANADADA asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo 'Aunty Lulu' amefukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Kinondoni jijini Dar es Salaam kutokana na mmoja wa wanaume aliokuwa akiishi nao anayedaiwa kuwa 'si riziki' kufumaniwa akifanuya uchafu chooni.
Akizungumza na Mpekuzi, mmoja wa majirani wa Aunty Lulu ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema mwanadada huyo pamoja na wanaume aliokuwa akiishi nao walifukuzwa wiki iliyopita na mwenye nyumba baada ya kubaini kuwa, wanatumia chumba chao kufanya ufuska. “Yaani sijui kwa nini Aunty Lulu alikuwa anawang’ang’ania wale watu, yaani walikuwa wanatusumbua kweli mpaka mwenye nyumba kaamua kuwafukuza, kitendo cha kufumwa chooni siyo cha mara ya kwanza, hii ni mara ya pili,” alisema jirani huyo.
MWAN
Baada ya kupata habari hizi, mwandishi alimtafuta Aunty Lulu ambapo alikiri kufukuzwa ndani ya nyumba hiyo kutokana na tabia za wanaume hao .
“Ni kweli, wale wanaume wameniharibia sana na sasa naishi kwetu huko Mbezi wakati natafuta chumba kingine,” alisema Aunty Lulu.