"MUZIKI UNALIPA ZAIDI KULIKO FILAMU NA MAIGIZO"......SHILOLE

 Msanii anaefanya vizuri kwa sasa kwenye muziki wa mduara Shilole, amesema kuwa ndani ya mwaka huu 2012 unaoelekea kuishia tasnia ya muziki imemlipa kwa kiasi kikubwa na kumpa mafanikio kwa haraka kuliko filamu tasnia ambayo ndiyo iliyomtambulisha kwa mashabiki.
Mwandishi wetu alizungumza na msanii huyo ili kujua kati ya filamu na muziki ni tasnia ipi ambayo anaweza kusema imemlipa kwa kiasi kikubwa, ndipo alipotaja muziki kuwa umeweza kumjenga kimaisha sambamba na kujulikana karibu duniani kote.


Alisema kuwa faida kubwa aliyoipata kwenye muziki ni kwamba alikuwa hakosi show na kila show anayopiga huwa analipwa kiasi kikubwa cha pesa, tofauti na filamu ambazo hucheza mara moja na kusubiri ifanye vizuri sokoni.

“Muziki kwa namna moja ama nyingine umejenga maisha yangu kwa kiasi kikubwa sana naweza kusema ni tasnia ambayo imenipa mafanikio makubwa sana namshukuru mungu kwa kunipa kipaji cha kuimba na uwezo kila siku, pia nawashukuru mashabiki wangu kwa kunikubali na tangu nilipotoa wimbo wangu wa kwanza,” alisema.

Hata hivyo aliulizwa swali kuwa ndani ya mwaka huu amecheza filamu ngapi za kwake mwenyewe, ndipo alipojibu kuwa hajatoa filamu yake mwenyewe hata moja na zote alizocheza zilikuwa za kushirikishwa lakini anaamini hapo mwakani atakuja na project yake mwenyewe ya kutoa movie kutoka kwenye kampuni yake.

“Ndani ya mwaka huu kwa kweli sijatoa movie yangu mwenyewe na zote nilizofanya nilikuwa nashirikishwa lakini najipanga kuja na project yangu mwenyewe hapo mwakani Mungu akipenda na hiyo ndiyo itakuwa safari yangu mpya kwani nitakuwa natoa kazi kutoka ndani ya kampuni yangu,” aliongeza.

Hii  ni moja  ya  kazi  zake.......

Posted by Bigie on 12:28 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.