"MBWA WANGU HUNIONDOLEA MAWAZO NA KUNIFARIJI"....JOHARI
BONGO MOVIE, habari za kitaifa, JOHARI 12:09 AM
STAA wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kuwa anapokuwa nyumbani kwao marafiki zake wakubwa ni mbwa wake wawili ambao anawafuga kwa sasa.
Akiongea kwa kujiamini, Johari alisema kuwa mbwa hao huwa wanamsaidia pindi anapokuwa na mawazo kwani humchangamsha pale anapocheza nao.
“Unajua nawapenda sana mbwa wangu na sijui ni kwa nini nilichelewa sana kuwatafuta, mara nyingi hunifariji wakati ninapokuwa na mawazo mabaya,” alisema Johari.
Mbali na mbwa hao, pia Johari alisema kuwa siku mojamoja huenda kuchungulia katika bendi mbalimbali za burudani kwa ajili ya kuchangamsha akili yake.A
Posted by Bigie
on 12:09 AM.
Filed under
BONGO MOVIE,
habari za kitaifa,
JOHARI
.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0