Waliohujumu CHADEMA Watimuliwa
news 6:01 PM
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewatimua wanachama wake 42 wakiwemo wagombea walioshindwa kupita kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.
Kwa
mujibu wa taarifa ya chama hicho, kutimuliwa kwa wanachama wake hao ni
hatua ya chama hicho kujisafisha kutokana na kile kinachodaiwa kwamba
baadhi ya wagombea hao wanatuhumiwa kufanya hujuma wakati wa mchakato wa
uchaguzi serikali za mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14,
mwaka huu.
Akitangaza
uamuzi huo mjini humo, Katibu wa Chadema Jimbo la Korogwe Mjini,
Ezekiel Mbwilo alisema wahusika waliotimuliwa uanachama wanatuhumiwa kwa
kukubali vitisho na wengine kurubuniwa kwa fedha za wapinzani wao,
hatua iliyowalazimu kwenda kuondoa majina yao katika hatua za mwisho
kuelekea kwenye kinyang’anyiro hicho.
“Tuligundua
kuwa baadhi ya wahusiska walijihusisha na hujuma mbalimbali dhidi ya
chama chetu, ikiwamo kukubali kupewa fedha na wapinzani wao ili
wajiondoe. Tangu awali, tulishakubalina kwamba ikibainika watu
waliofanya hujuma tutawatimua kundini na hapa ndipo tunahitimisha lile
tulilokubaliana,” alisema.
Mbwilo
alitaja maeneo wanayotoka wanachama hao waliotimuliwa na idadi yao
kwenye mabano ni Kwamsisiwatu (6), Mahenge (10), Kitifu (25) pamoja na
mmoja kutoka Manundukati ambaye alidai kwamba mhusika huyo aliamua
kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi ukiwa katika hatua za mwisho
baada ya kurubuniwa na wapinzani wa chama hicho.
Akizungumzia
vitisho alivyodai vilitolewa baadhi ya wanachama wa vyama vingine dhidi
ya wagombea wa Chadema, Mbwilo alisema tayari amewasilisha taarifa hizo
kwenye vyombo vya usalama na katika jeshi la Polisi kwa ajili ya
uchunguzi.