BERENIKI KIMARO NDIYE MSHINDI WA "MAISHA PLUS 2012"
Posted by Bigie habari za kitaifa, maisha plus 8:20 AM Mshindi wa Maisha Plus 2012 kutoka Dar es salaam ni BERENIKI KIMIRO, amejishidia Tshs. Millioni 20.
BERENIKI KIMIRO alianza kwa Kumshukuru Mungu kwa ushindi, amsema ye si kitu kwa wenzake, hilo ni zali tu.. Amemshukuru baba yake mzazi kwa kumshauri kusali. Aliwashukuru pia wapenzi watazamaji kwa kumpiga kura, ameahidi kuendeleza kile alichokianzishaa kijijini na kuitendea haki nchi yake
Alimshukuru babu, Brother Masoud na Crew nzima ya Maisha Plus.. Alimshukuru pia mwanae Kelvin (6yrs) kwa kuvumilia kipindi chote bila kuongea na mama. Alisema Mungu amejibu maombi yake kwani ukipiga goti, maombi yako yatajibiwa..
Mshindi wa Pili ni Venance Mushi kutoka Dodoma amejishindia Tshs. Million 6.
Mshindi wa Tatu ni Justine Bayo, kutoka Morogoro amejishindia Tshs. Million 4.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu aliitwa kusema machache pamoja na kutangaza Mshindi wa Maisha Plus 2012.. Masoud Kipanya, alimkaribisha, akishukuru kwa zawadi aliyoitoa ya ya Tshs. Millioni 10 ambayo itagawanyika Millioni 6 kwa Mshindi wa Pili na Million 4 kwa mshindi wa tatu.
Mhe. Nyalandu aliongezea zawadi ya Tshs. Million 7.5 ili igawanywe Tshs. Laki tano kwa kila mshiriki ambaye hakuingia top 3, aliwakaribisha pia washiriki wote kwa chakula cha Mchana siku ya kesho katika hoteli ya Serena.
HATIMAYE KIJIJI CHA MAISHA PLUS CHAZINDULIWA
Posted by Bigie habari za kitaifa, maisha plus 1:02 AMNaibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, jana wamezindua shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2012.
Uzinduzi huo umeshuhudia wanawake 14 waliongia kambini kwenye kijiji cha Maisha Plus ambao baadaye wataungana na vijana watakaoshiriki kwenye shindano la Maisha Plus.
Akizungumza baada ya kuwatambulisha Mama Shujaa 14 watakaoshiriki kwenye shindano hilo kumpata mshindi mmoja, Mheshimiwa Malima alisema serikali itahakikisha kuwa mwanamke ambaye ni mzalishaji mkuu wa chakula kwenye jamii ya Tanzania anawekewa mazingira mazuri ambayo yatasaidia shughuli za kilimo ziwe na tija zaidi.
Kwa upande wake Mheshimiwa Mwalimu alisema wanawake wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi kwenye jamii ambapo pamoja na kushiriki katika uzalishaji wa chakula wamekua wakikosa mamlaka na uamuzi wa kile wanachokitayarisha kutokana na kuendelea kuwepo kwa mfumo dume ambapo mwanaume huwa juu ya mwanamke.
Alisema wanatambua kuwa kipato kinachopatikana kutokana na shughuli za kilimo kinamilikiwa na wanaume ambapo pia wanawake wengi hawamiliki ardhi.
Aliongeza kuwa serikali inazitambua changamoto hizo na inafanya kazi kuziondoa kabisa.
Mheshimiwa Mwalimu alisisitiza kuwa shindano la Mama Shujaa lengo lake ni kuikumbusha jamii umuhimu wa mwanamke katika uzalishaji wa chakula na kwamba sheria inasema mwanamke na mwanaume wana haki ya sawa katika maamuzi ya kile wanachozalisha.
Naye Mkurugenzi mkazi wa shirika la OXFAM ambalo ni wadhamini wa shindano hilo Bi. Monica Gorman alisema wanawake ni waendeshaji wa uchumi wa Tanzania lakini umuhimu wao umefunikwa kwa muda mrefu hivyo kwa kutumia shindano la Mama Shujaa wa Chakula, wanawake wanamulikwa ili wapate kile wanachostahili.
Shindano hilo lina lengo la kuwainua wanawake, kuwapa moyo na kuwaunga mkono wakulima wadogo wanawake nchini na kuongeza kukubalika kwa mchango wao katika kilimo.
Uzinduzi wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2012 ulioneshwa live kupitia kituo cha TBC1.
USAILI WA MAISHA PLUS 2012 DAR WAVUNJA REKODI......
Posted by Bigie habari za kitaifa, maisha plus 11:53 AMZile auditions za reality show ya Maisha Plus 2012 ambayo tayari imeanza kuruka kupitia TBC1 kila siku kuanzia saa 4 usiku, zimefanyika jana pale Millenium Tower.
Hivi ndivyo watu walivyojitokeza kwa wingi katika auditions hizo. Waandaaji wanasema walitarajia kupata washiriki wengi lakini hawakutegemea wangekuwa wengi kiasi hiki hivyo idadi hii kubwa ya waliojitokeza hapo jana imevunja rekodi.
Leo ni siku ya pili ya auditions hizo ambazo zilipangwa kufanyika kwa siku mbili.
USAJILI WA MWISHO WA MAISHA PLUS UTAFANYIKA JUMATATU SEPTEMBA 24
Posted by Bigie habari za kitaifa, maisha plus 11:25 AMNafasi ya mwisho ya kuaudition kwa ajili ya kushiriki shindano la Maisha Plus itafanyika jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu, Septemba 24 pale Millenium Tower, Kijitonyama.
Wale waliochukua fomu na ambao bado hawajachukua, wafike Millenium Tower ghorofa ya kwanza waulizie KP Shop.
Kwa wale wenye ndoto ya kushiriki katika shindano hili mwaka huu, Jumatatu ndio itakuwa siku ya mwisho kujaribu bahati yao kwani ukiikosa itabidi usubiri mpaka mwakani.
Kwa wapenzi wa shindano hili stay glued to TBC1 kwasababu soon burudani itakufuata sebuleni kwako.
.
Featured Post
NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...


