WEMA SEPETU AKIRI KUTOKUWA NA WIVU JUU YA DIAMOND.
JAMII 5:18 AM
Diva anayefanya kweli ndani ya Bongo Movies Industry, Wema Issack Sepetu amefunguka kuwa, hana wivu kwa mpenzi wake anaye-shine kinoma kunako gemu la muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Akitema cheche mbele ya mpekuzi wetu, juzikati jijini Dar es Salaam, Wema alisema haoni sababu ya kuwa na wivu sana na Diamond kutokana na ‘nature’ ya kazi yake ilivyo.
“Ni vigumu lakini mimi nimeji-control na nimeweza.
Hata kama nikijifanya nina wivu nitajitesa tu. Yeye ni msanii, mara nyingi anakwenda kwenye matamasha, wakati mwingine anasafiri mikoani, navumilia,” alisema Wema na kuongeza:
“Jambo kubwa ninalitegemea ni penzi langu la dhati kwake naye kwangu.
Hawezi kufanya chochote, ndiyo maana nampa uhuru.
Nampenda sana Diamond wangu, lakini sioni kama wivu ni silaha ya kumlinda, penzi linatosha.”






