AISHA MADINDA AKIRI KUWA " MOYO WAKE BADO UPO KWA DANGER BOY"


Mnenguaji  ghali Bongo, Aisha Mbegu ‘Madinda’  (pichani) anayepiga mzigo ndani ya Bendi ya Extra Bongo, ameibuka na kueleza hisia zilizopo moyoni mwake juu ya mcheza shoo anayefanya naye kazi, Isaack Buruhani ‘Danger Boy’.

Akizungumza naWAPEKUZI  juzi jijini Dar es Salaam, Aisha alisema tangu alipoachana na Danger Boy amekuwa wa kuhangaikia sana kimapenzi na hajawahi kupata pumziko la kweli.

Sijapata penzi la kweli kama nililokuwa nikipata kwa Danger, alikuwa na upendo wa kweli. Alinifanya hadi nikaachana na wanaume wote waliokuwa wakinisaidia kifedha kwa ajili yake.

Ni mwanaume anayejali sana, aliwapenda wanangu kama wake na kuna wakati alikuwa akiwapeleka shuleni. Nimeomba sana ushauri kwa watu mbalimbali, wameniambia nirudi kwake, hapa nilipo nafikiria namna ya kwenda kuzungumza naye,” alisema Aisha na kuongeza:

Anatakiwa ajue nampenda sana, hata yeye naamini ananipenda pia. Anakumbuka nilifikia hatua ya kuachana na Fikiri (Madinda) kwa ajili yake. Bado nampenda, nitakaa naye nimweleze yangu ya moyoni.”

Posted by Bigie on 12:10 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.