BASI LA ABOOD LAPATA AJALI ILIYOSABABISHWA NA MWENDO MKALI. ABIRIA ASIMULIA MKASA HUU KWA UCHUNGU



    
    ABIRIA ALIEKUWA KATIKA BASI LA  "GREEN STAR" ALISHUHUDIA AJALI HII NA KUNISIMULIA KAMA IFUATAVYO:-

   Habari ndugu MPEKUZI!! Pole na shughuli za ujenzi wa Taifa
 
  LEO (ambayo ni jana) nilikuwa nasafiri kuelekea Mbeya .Namshukuru mungu nimefika salama . Hata hivyo kumekuwepo na matukio kadhaa ya kusikitisha hasa mwendo kasi wa mabasi .
    Ilikuwa ni kama saa tisa hivi mara baada ya kupita Mafinga mkoani Iringa ndipo tulipoingia katika msitu wa Sao hill, tukiwa katika msitu huo kabla hatujaumaliza lilikuja basi la Abood lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda Mbeya likienda kwa kasi ya ajabu, kila aliyekuwa kwenye basi la Green Star nililokuwa nimepanda aliushangaa mwendo wa dereva yule ambaye jina lake halikupatikana mara moja. 
 
   Mara baada ya kupita eneo la Nyororo kama kilomita 20 hivi kwenye mteremko yalikuwa yameongozana mabasi mawili ambayo ni Super Feo linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam Songea huku nyuma basi la Abood likifuata kwa kasi ya ajabu. Wakati dereva wa basi la Super Feo akijaribu kulipita roli lililokuwa mbele yake likielekea Mbeya ghafla mbele yake, aliona kuna roli lingine lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es salaam likiwa limeharibika barabarani, hivyo ikabidi achukue tahadhari ya kusimama ghafla.
 
    Wakati akisimama tayari basi la Abood lilikuwa limeshamfikia na kushindwa kusimama kutokana na mwendo wa kasi hivyo likaligonga basi la Super Feo kwa nyuma, na kujeruhi watu kadhaa akiwemo Dereva huyo ambaye alibanwa na usukani kama anavyoonekana hapo  juu  na chini wasamaria wema wakijaribu kung'oa mabati ya basi hilo ili kumnasua



Posted by Bigie on 11:41 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.