AUNT LULU APARAMIA POMBE NA KUFANYA MAMBO YASIYO NA HESHIMA HADHARANI
JAMII 5:21 AM

Mtangazaji mahiri wa Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amenaswa akiwa hoi kwa kilevi na kuwaacha wadau midomo wazi
Kituko ni kwamba, Aunty Lulu alifakamia pombe hizo zilizompeleka hali ya ‘u-tilalila’ katika kipindi hiki ambacho anakabiliwa na mitihani ya kumaliza masomo ya uandishi wa habari ngazi ya stashahada.
Staa huyo aliyeanza ‘kuhiti’ tangu akiwa na umri mdogo, alinaswa na MPEKUZI wetu usiku wa Jumatano iliyopita ndani ya Club Bilicanas, Dar es Salaam.
Ilikuwa saa 6:39, ambapo mpekuzi wetu alimtia machoni Aunty Lulu kwa mara ya kwanza ndani ya klabu hiyo, kulikokuwa na shoo ya Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.
Baada ya kuzunguka kwa dakika mbili hivi, Aunty Lulu alitenga makalio jirani na moja ya kaunta za klabu hiyo na kuanza kupiga pombe ambayo ilimchakaza na kumuacha hoi.
Kama ilivyo kwa msemo, ‘ulevi noma, funda moja tu la ziada linaweza kukuumbua’ ndivyo mambo yalivyomtokea puani Aunty Lulu, kwani mwisho alikuwa taabani na kufanya yasiyo na heshima.
Baada ya kupigiwa simu siku ya alhamisi ili kumjulia hali kutokana na jana yake kuwa tilalila alijibu: “Jamani mimi sikumbuki kitu, rafiki zangu ndiyo wameniambia asubuhi hii. Nadhani pombe sasa zinanishinda, hii ni hatari.”









