MASOMO YANANIPUNGUZIA STAREHE--ASEMA TEDDY

MSHIRIKI wa shindano la Maisha Plus season I, Tereza John ‘Teddy’,  amefunguka kuwa, masomo yamempunguzia starehe kutokana na  kushindwa kwenda viwanja mbalimbali kwa ajili ya ‘kula bata’ kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Akiongea na MPEKUZI wetu  juzikati jijini Dar, Teddy alisema kutokana na kubanwa na ratiba za masomo analazimika kutumia muda mwingi kufanya kazi anazopewa chuoni na kukosa muda wa kwenda kujirusha.


“Unajua mimi ni mtu wa starehe, lakini kwa sasa imebidi ninyooshe mikono kutokana na kubanwa na ratiba za masomo hapa chuoni,” alisema mrembo huyo.


Teddy yupo chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam ‘DSJ’ akiwa mwaka wa mwisho wa masomo ya Stashahada.

Posted by Bigie on 4:07 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.