HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA YALAUMIWA KWA UZEMBE ULIOSABABISHA KIFO CHA MFANYAKAZI WA STUDIO YA PHOTO NEX
JAMII 11:22 PM
Wapiga picha katika Manispaa ya Iringa wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Issa Mwamba aliyekuwa mfanyakazi wa Studio ya kuosha picha ya Photo Nex
Ndugu hao waliuambia mtandao huu kuwa marehemu kabla ya kifo chake alianguka eneo la duka la Pera na kukimbizwa Hospital ya mkoa na baada ya kufika wauguzi waliishia kumtazama bila kutoa msaada na baada ya muunguzi aliyekuwepo kuombwa namba ya mganga mkuu wa hospital hiyo walinyimwa.
Hata hivyo walisema kutokana na kukosa msaada huo walilazimika kwenda kituo cha polisi ili kuomba msaada na baada ya kurudi walikuta mgonjwa wao amepoteza maisha.
Ndugu hao wamepanga kufika kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma kufikisha kilio chao dhidi ya utendaji wa wauguzi wa hospital ya mkoa wa Iringa ikiwa na kuzungumza na wanahabari ili kusaidia kufuatilia suala hilo.






