CAG :: OFISI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI YAPANGA KUFANYA UKAGUZI WA ZIWA VICTORIA



   ZIWA VICTORIA linatarajiwa kufanyiwa ukaguzi na ofisi ya mkaguzi  mkuu wa serikali hapa nchini(CAG) kwa kuwa imebainika kuwa ziwa hilo  linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya uharibifu wa  mazingira.

     Hayo yamebainishwa na mkaguzi mkuu katika ofisi hiyo Bw Ludovick  Utouh wakati akiongea na wadau mbalimbali wa mazingira kutoka katika  nchi mbalimbali duniani ambapo mkutano huo unaendelea mjini arusha.

   Bw Utouh alieleza kuwa kwa sasa ziwa victoria lina changamoto  mbalimbali ambapo ofisi yake inatakiwa kufanya ukaguzi mara moja kw  maslahi ya taifa la nchi hii.

     Mkaguzi huyo alisema kuwa ziwa hilo ambalo ni kitega uchumi kikubwa  sana kwa wananchi wa maeneo hayo kinakisha kutokana na kuwepo kwa  changamoto za uharibifu wa mazingira.

   Moja ya changamoto ambayo Mkuu huyo ameitaja ambayo imefanya kuwepo  na ukaguzi ndani ya ziwa hilo ni pamoja na changamoto ya uhaba wa  samaki ambapo idadi ya samaki ndani ya ziwa hilo imepungua sana tofauti  na miaka ya nyuma ambapo kuikuwa na samaki wengi sana.       "ofisi yangu itafanya mkakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa  inakagua ziwa victoria ambapo katika ukaguzi huo pia tutabini chanzo  halisi ambacho kimefanya kuwepo na samaki wachache na tutatoa tathimini  kubwa sana kwa kuwa lile ziwa ni mali ya umma"alisema Utouh

   Mbali na ukaguzi huo ndani ya ziwa victoria mkaguzi huyo alisema  kuwa watafanya kaguzi mbalimbali katika misitu ambayo nayo ni mali ya  umma ambapo napo wataweza kutoa tathimini halisi la  misitu hiyo.

   Naye waziri katika ofisi ya raisi ktengo cha mazingira Dkt Terezya  Luoga alieleza kuwa mpango huo wa ukaguzi ambao ni mpya kabisa hapa  nchini utakuwa na tija kubwa ya kuweza kuwasaidia wananchi katika  kuhifadhi mazingira

   Dkt. Terezya alibainisha kuwa ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali  inatakiwa kuwataja kwa majina hadharani makampuni,mashirika, pamoja na  watu binafsi ambao wataonekana kama chanzo mojawapo cha ubadilifu wa  mazingira hasa katika ziwa hilo na ndani ya misitu.

   Dkt huyo alibainisha kuwa endapo kama walengwa ambao wanasababisha samaki kufa  ndani ya ziwa watatajwa hadhari ni wazi kuwa hata shuguli haramu za  uharibifu wa mazingira zitapungua kwa kiwango kikubwa sana tofauti na  sasa ambapo hamna kaguzi zozote kutoka serikalini.

Posted by Bigie on 9:21 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.