MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLYA YA KUANZISHA BLOG


Habari  wapenzi wasomaji wa blog ya MPEKUZI. Leo nimeona nizungumze na  Watu wanaotaka kuanzisha BLOG

  MAANA YA BLOG
      BLOG ni website ndogo ambayo hutumiwa  kwa taarifa mbalimbali kama MICHEZO,HABARI,MZIKI,FASHION na mengine mengi..Tofauti iliyopo kati ya blog na WEBSITE  ni kuwa BLOG  mara nyingi ina  "Limited Pages" nikiwa na maana kuwa ina idadi maalum za kurasa na HAIHITAJI UWE NA DATABASE

FAIDA ZA KUWA NA BLOG
      Blog mara nyingi ziko HOSTED (zimewekezwa / zinasimamiwa) na BLOGGER  au WORDPRESS ambao hutoa huduma hii BUREEEE.Ninacho maanisha ni kuwa HAKUNA MALIPO YOYOTE
      Kwa mantiki hii,BLOG imekuwa kitega uchumi kizuri hasa kwa nchi zinazoendelea na baadhi ya nchi kama NIGERIA.Wanatengeneza hela nzuri sana kiasi kwamba mtu anafikia hatua ya kutoona haja ya KUAJILIWA TENA.

MAMBO MATATU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BLOG
        Kabla hujaanzisha blog yoyote,ni lazima ukae chini ujiulize LENGO la kuwa na blog ni nini!!!!.  Usianzishe blog kwa kuwa tu wengine wana blog pia.,HAPANA,utakuwa unapoteza muda na pengine ni bora ukafanya mambo mengine ya msingi zaidi.Yafuatayo ni mambo makuu matano yakuzingatia
   
  1. FIKIRIA NAMNA YA KUWATEKA WASOMAJI
             Kitu cha kwanza kabisa ni lazima ufikirie juu ya wasomaji..Jiulize ni nani ataeyeitembelea BLOG yako.kwa kufanya hivyo itakusaidia kujua na kupanga juu ya habari za kuweka katika BLOG yako.Ifanye blog yako iwe na MUONEKANO MZURI,kiasi kwamba mtu akiitembelea siku moja atatamani na kesho arudi tena hata kama  huna habari nzuri ulizoandika.

  2. NI VIZURI KILA HABARI IKAWA  NA PICHA.
         Picha hubeba ujumbe mkubwa sana mana ni kielelezo tosha kabisa cha taarifa unayozungumzia. Huwezi ukasema kwa mfano " mpekuzi akutwa baa"  bila kuwa hata na picha moja inayothibitisha kuwa ni kweli mpekuzi amenaswa baa!!  .Wafanye wasomaji wako wakuamini.Lakini pia ni lazima picha yako iwe na muonekano mzuri

3. JITAHIDI BLOG YAKO IWE NA MUONEKANO MZURI

    Hapo mwanzo nilisema kuwa HUDUMA YA KUWEKEZA BLOG NI BURE. Ni kweli kabisa lakini  kuna gharama ndogo wakati wa utengenezaji wake.Ninacho maanisha ni kuwa,ni lazima umtafute mtu mwenye ujuzi wa HTML  na JAVASCRIPT ili akutengenezee blog yenye " interface nzuri".Vinginevyo utaishia kuwa na blog ambayo haina wasomaji.Gharama ya kuanzisha na kutengeneza blog inategemea na mtu mwenyewe.Hakuna bei maalum.Kama utaridhia toka moyoni kuwa unataka kuwa na blog,basi usihangaike.MIMI PIA NI MJUZI NA MTAALAM WA KUTENGENEZA BLOGS NA WEBSITE.  Kwa kuwa lengo langu ni kuwaelimisha  wenzangu ili nao wanufaike na huduma hii,basi,ntakufanyia bei ya kubinadamu sana ambayo najua huwezi amini.Lengo langu ni kukusaidia na si kukuumiza

  MAADA ITAKAYOFUATA::>>   MBINU ZA KUTENGEZA PESA KUPITIA BLOG

Kama unaswali lolote juu ya BLOGS ,naomba uandike maoni yako hapo chini nami ntakujibu na kukuelimisha zaidi.Na kama umeguswa na MAADA hii na hivyo umepanga kuanzisha blog,basi usiste kuwasiliana na mimi.kama nilivyokuahidi,lengo langu ni kukusaidia na si kukuumiza.
Niandikie sms : 0754722937  au  nitumie email:   jozzbenard@yahoo.com
  
ANGALIZO:   Kama una swali,naomba uniulize kwa njia ya maoni hapo chini badala ya kuniandikia sms au email


Posted by Bigie on 8:58 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.