CHADEMA WAFANYA VURUGU NA KUTEKETEZA GARI LA DIWANI KWA MOTO


Wafuasi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Wilaya ya Igunga na Moshi Vijijini,  jana wamefanya vurugu ikiwemo kuteketeza gari la diwani kwa moto, wakipinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika juzi.

Mjini Igunga, hali ya amani jana ilichafuka baada ya kundi la vijana wanaodaiwa kuwa ni wa Chadema kuanza vurugu za kupita wakiimba katika mitaa mbalimbali mjini humu wakidai matokeo ya ubunge yatangazwe haraka.


Saa moja asubuhi siku ya jana , vijana hao wakiongozwa na gari la matangazo la Chadema walipita katika

barabara kuu ya Igunga wakitangaziwa kuwa chama hicho kimeshinda.

Wakati vijana hao wakifanya vurugu hizo na kusababisha huduma zote za jamii kufungwa katika mji huo, tayari baadhi ya viongozi wao akiwemo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Godbless Lema wa Arusha Mjini walikuwa wameshatoa matamko ya kukubali kushindwa.


Pamoja na viongozi wa Chadema kuwa tayari wamekubali kushindwa, MPEKUZI alishuhudia

vijana hao wa Chadema wengi wakiwa wageni katika Hoteli ya Peak walipokuwa viongozi wa
CCM, wakirusha mawe na kupasua kioo cha moja ya magari ya chama hicho na kusababisha vijana wa CCM kutoka nje kuwakabili. 
MPEKUZI wetu pia alishuhudia vijana wengine wa Chadema wakijikusanya katika Halmashauri ya
Wilaya ya Igunga wakidai matokeo ya uchaguzi huo kwa mawe na kuanza kuchoma moto majani makavu yanayozunguka ofisi hiyo, hali iliyosababisha Polisi kuingilia kati kwa kuwatawanya kwa maji ya kuwasha na mabomu ya machozi. 

Posted by Bigie on 9:38 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.