CCM YAMGEUKA MSHINDI WAKE WA IGUNGA PAMOJA NA MADIWANI WALIOSHINDA



Chama Cha Mapinduzi-CCM kimewataka viongozi waliochaguliwa katika Uchaguzi Mdogo na Ubunge na Udiwani kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho.

Mbali na hilo Chama kimewapongeza wananchi wote wa Igunga kwa kumchagua Dokta PETER KAFUMU kuwa Mbunge wao pamoja na wananchi katika Kata 17 ambazo CCM imeshinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Udiwani.

Katibu wa NEC wa CCM Itikadi na Uenezi Ndugu NAPE NNAUYE (pichani)katika mkutano wake leo na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam amesema Chama kitakuwa karibu na Wateule hao ili kuhakikisha kuwa wanawajibika kikamilifu kwa wananchi waliowachagua.

Kutokana na ushindi huo Chama Cha Mapinduzi katika maeneo mbalimbali nchini kimeandaa mikutano ya hadhara ya kuwapongeza wananchi kwa kuichagua CCM katika chaguzi hizo ndogo zilizofanyika Jumapili iliyopita.

Kwa mujibu wa Ndugu NAPE leo kutakuwa na mkutano wa hadhara utakaoongozwa na viongozi wa Sekriterieti ya CCM huko Mkoani Singida ambapo keshokutwa kutakuwa na mkutano Mjini Dodoma.

Octoba Saba mwaka huu kutakuwa na mkutano wa hadhara Mjini Kibaha na siku inayofuata ambayo ni Jumamosi kutakuwa na mkutano mkubwa jijini Dar es salaam utakaohudhuriwa pia na Mbunge Mteule wa Jimbo la Igunga Dokta KAFUMU.

Posted by Bigie on 5:42 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.