MAPIGANO MAKALI YAZUKA BAADA YA MELI YA UTAFITI WA MAFITA NCHINI TANZANIA KUSHAMBULIWA NA MAHARAMIA.

Kituo cha utafutaji na uokoaji majini (MRCC) kinachoratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kimepokea taarifa za kushambuliwa kwa meli ya utafiti wa mafuta iitwayo Ocean Rig Poseidon. Tukio hilo limetokea tarehe 3/10/211 saa 2:15 usiku, umbali wa maili za baharini 23 kusini mashariki ya kisiwa cha Mafia sawa na maili 82 kutoka Dar es salaam.
Katika tukio hilo maharamia 7 waliokuwa katika boti ndogo waliishambulia meli hiyo kwa silaha. Mashambulizi hayo yalijibiwa na walinzi wa meli na Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na maharamia walidhibitiwana kukamatwa na wanashikiliwa mikononi mwa jeshi la Wanamaji.

Posted by Bigie on 5:19 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.