CHAWATA - MBEYA YAITAKA SERIKALI KUJENGA MIUNDO MBINU ITAKAYO WAWEZESHA WALEMAVU KUPATA HAKI ZAO ZA MSINGI
JAMII 7:15 PM
Serikali, makampuni wa wadau mbalimbali wa masuala ya ujenzi nchini wametakiwa kujenga majengo kwa kuzingatia kuweka miundombinu sahihi ambayo itawawezesha walemavu kupata haki zao za kimsingi au huduma halali katika majengo hayo.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu mwenyekitio wa Chama cha walemavu Tanzania ndani ya mkoa wa Mbeya (CHAWATA) Bwana Jimmy Ambilikile wakati wa mahojiano maalum na MPEKUZI wetu
Amesema iwapo majengo ya huduma muhimu yatajengwa kwa kuzingatia mazingira ya kundi hilo maalumu yatawezesha malemavu kupata huduma zao bila usumbufu wa aina yoyote.
Walemavu wamekuwa wakishindwa kufikia huduma muhimu za kijamii kutokana na makandarasi wa ujenzi kutojenga majengo yao kwa kutokufikilia kundi hilo maalumu.
Aidha uchunguzi uliofanywa na kundi la WAPEKUZI umebaini kuwa ofisi mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha, afya na vyuo havina na miundombinu bora inayowawezrsha walemavu kupata huduma zao kwa urahisi.






