TRANSFORMER YALIPUKA NA KUWAKA MOTO KATIKA KITUO CHA UTANGAZAJI CHA TBC
JAMII 5:13 AM
TRANSFOMA ya umeme iliyoko katika kituo cha Tasisi ya Utangazaji cha Taifa (TBC) Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ililipuka na kuwaka moto leo asubuhi majira ya saa tano wakati mafundi wakiifanyia marekebisho. Tukio hilo lilisababisha tafrani kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo na kampuni ya Star Time yenye ofisi zake ndani ya taasisi hiyo, na maeneo ya jirani.
Fundi mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana, alikuwa juu akifanya matengeenezo hayo ambapo aliungua vibaya kwa moto na kukimbizwa hospitalini.
Mmoja wa wafanyakazi wa Star Time akitafuta mbinu zaidi.
Baadhi ya watu waliofika eneo la tukio.
Gari la zimamto la Knight Support likiingia kuudhibiti moto huo.
Wafanyakazi wa Knight Support wakiuzima moto.










