MBUGE WA MBALALI MKOANI MBEYA ATIWA MBARONI KWA ULINZI MKALI
JAMII 4:10 PM
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Habari zilizotua hivi punde katika mtandao huu kutoka Mbarali mkoani Mbeya zinadai kuwa hali ya mambo si shwari ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Mbarali mkoani Mbeya baada ya mbunge wa jimbo hilo Mheshimiwa Dickson Kilufi kukamatwa na jeshi la polisi na kusindikizwa mjini Mbeya kwa ulinzi mkali jioni ya ijumaa kuamkia leo jumamosi.
Mbunge huyo amekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kutishia kuua kwa bastola .
Mbunge huyo amekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kutishia kuua kwa bastola .
Imedaiwa kuwa mtego wa kumnasa mbunge huyo uliwekwa na jeshi la polisi mapema leo na kufanikiwa kumnasa mbunge huyo na kumpeleka polisi kwa ulinzi mkali na hadi sasa yupo chini ya ulinzi wa polisi
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocete Nyombi ameuthibitishia mtandao huu kuwa ni kweli mbunge huyo yupo chini ya mikono ya sheria kwa tuhuma za kutishia maisha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocete Nyombi ameuthibitishia mtandao huu kuwa ni kweli mbunge huyo yupo chini ya mikono ya sheria kwa tuhuma za kutishia maisha.