MTOTO AZALIWA AKIWA NA SURA MBILI: MADAKTARI WAPIGANIA KUYAOKOA MAISHA YA MTOTO HUYU


Madaktari  wa Hospitali ya  Holy Family (HFH) mjini hapa wanapigania maisha ya mtoto aliyezaliwa Septemba 25, mwaka huu akiwa na sura mbili na uzito wa kilo 3.2.

Kwa mujibu wa taarifa za hospitalini hapo, mtoto huyo mara baada ya kuzaliwa amekutwa ana tatizo la kupumua hivyo kumlisha kupitia mdomo, mpashaji aliliambia Gazeti la The Express Tribune.

Mtoto huyo ni wa tatu kuzaliwa  kutoka kwa Bi. Shahida Perveen na mumewe Khalil Ahmed. Msajili wa hospitali hiyo, Dk. Qaisar Aziz ameliambia The Express Tribune kwamba mtoto huyo amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit) katika wodi ya watoto na atakuwa katika uangalizi wao.

 Hata hivyo, madaktari wameonesha kukata tamaa na kusema kuna uwezekano mdogo kwa mtoto huyo kuendelea kuishi na kukua. “Kumlisha kwa kutumia mdomo haiwezekani kwa sasa, tunamlisha kwa kutumia mipira maalum (Naso-gastric tube). Sura hizi mbili zinafanana,” alisema Dk Qaisar.

Mtoto huyo ana macho manne, pua mbili, midomo miwili na masikio manne, kwa maana kwamba ana sura mbili.
Habari zinasema mama wa mtoto huyo alipopimwa na mashine maalum, (Ultrasound) alionekana hana matatizo yoyote na alikuwa na afya njema.

Posted by Bigie on 12:07 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.