STEVEN KANUMBA ASUMBULIWA NA TATIZO LA "PERSONALITY DISORDER" AMBAPO TIBA YAKE YATAJWA KUWA NI USHAURI NASAHA



Steven Charles Kanumba ni staa mkubwa Bongo. Jina lake kwa sasa lina hadhi ya kimataifa. Inawezekana akawa ndiye msanii kijana mwenye mvuto kijamii kuliko mwingine yeyote.

Mvuto wake unatambulika ndiyo maana makampuni mengi ya kibiashara na kijamii hupenda kumtumia kama balozi wao. Kanumba ni fahari ya Tanzania, ni kivutio cha vijana wengi wa kizazi kipya.
Pamoja na sifa nyingi alizonazo kuna makosa machache huwa anayafanya, hivyo anahitaji kupokea ushauri ambao utamsaidia kuepuka visa vya hapa na pale ambavyo humvunjia heshima.

UTANGULIZI
Hapa kuna baadhi ya matukio ambayo yamewahi kuripotiwa, hivyo kumchafua Kanumba, kwa hiyo anapaswa kujitenga nayo ili heshima yake ibaki kuwa juu.

1: Ugomvi na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu mpaka kufikia hatua ya kupelekana polisi.
2: Sylvia Shally alikuwa mpenzi wake lakini naye waligombana mpaka kufikishana polisi. Mrembo huyo alitinga ubaoni akidai Kanumba alimtishia maisha.

3: Alizama kwenye dimbwi la mahaba (kama alivyodai mwenyewe) na Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed. Walipoachana, alifunguka kuwa mrembo huyo ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, alikuwa anamtesa sana.
4: Anadaiwa kuwa na uhusiano wa siri na Aunt Ezekiel (ingawa wote wanakanusha), juzikati walitibuana, kisha yeye alimpa mitama mrembo huyo na kusababisha soo hilo litinge polisi.

MKASA MZIMA/USHAURI
Kwa nini kila siku ugomvi na wanawake? Inakuwaje polisi na yeye kwa makosa ambayo yana alama za kimapenzi?
Daktari aliye pia bingwa wa saikolojia, Godfrey Chale anadai kuwa tatizo linalomsumbua Kanumba linaitwa Personality Disorder na tiba yake ni ushauri na nasaha.
“Personality Disorder ina matawi mawili, inferior (kujihisi unyonge) na superior (kujiona unahitaji kuogopwa). Vitu hivyo hutengeneza wivu na migogoro mingi (conflicts).

“Mtu kama huyo atakuwa anajiona superior, kwa hiyo hujikuta ana chembechembe za dharau kwa kuamini ni maarufu na ni lazima mpenzi wake amnyenyekee. Ikiwa atakutana na hali tofauti, mfano akigundua mwenzi wake hafuati anavyotaka au anamsaliti, kwa kawaida hujisikia vibaya.

“Ile tabia ya kujiona superior ndiyo humfanya ashindwe kukubali matokeo hasi kutoka kwa mwenzi wake, kwani anaamini yeye ni mtu wa kunyenyekewa. Kutokana na hilo, ndiyo maana hupata kesi za kugombana au kusumbuana na wapenzi wake kwa sababu ya kutokubali matokeo,” alisema Dk. Chale ambaye ana hospitali binafsi,

Dokta Patrick Mirumbe wa Hospitali ya Capricorn alisema: “Tatizo lake ni wivu. Hiyo naweza kuzungumza kwa kifupi na tiba yake ni ushauri na nasaha. Akipata ushauri wa kutosha anaweza kubadilika na kuwa mtu safi.

HITIMISHO
Naamini kuwa maneno ya madaktari akiyashika sawasawa , bila shaka atashinda mitihani inayomkabili. Lengo ni kuona heshima yake inazidi kupaa juu na msimamo ni kwamba Kanumba bila polisi inawezekana.

Posted by Bigie on 12:47 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.