UTATA WATAWALA KATIKA UTAMBUZI WA MALI ZILIZOKUWA ZIMEIBIWA NA MPIGA NONDO ALIYECHOMEWA NYUMBA NA WANANCHI JANA
JAMII 9:40 AM
HIZI NI BAADHI YA MALI ZILIZOKUWA ZIMEIBIWA
Wananchi wa Manispaa ya Iringa mchana huu wanaendelea kutambua mali zao mbali mbali ambazo zikikutwa jana eneo la Kigamboni katika nyumba ya Msafiri Ilomo ambaye anadaiwa kumiliki mtandao wa ujambazi .
Wananchi wengi wameonyesha kukata tamaa kuendelea na kutambua mali zao baada ya kukosa ushahidi wa uhalali wa mali hizo baada ya wengi kufika kituo cha polisi bila ya risti za mali zao ,huku baadhi yao wakidai kukosa mali zao ambazo ziliibwa na wezi hao .
Baadhi ya vituko ambavyo vimejitokeza ni pamoja na kuwepo kwa nguo za ndani nyingi ambazo zinasadikika kuwa wezi hao walikuwa wakianua katika nyumba za wananchi ,pia bendera na skafu wa CCM pamoja na vitu vingine ambavyo ni mali ya makanisa na misikiti vimekutwa wakati wa utambuzi wa mali mbali mbali.
Wakati huo huo mmoja kati ya wanawake waliofika kutambua mali zilizoibwa ameueleza mtandao huu kuwa amepata kutambua nguo zake za ndani ambazo zilichukuliwa nawezi hao bafuni ,pamoja na nguo nyingine zilizokuwa zimeanikwa nje .






