WANAFUNZI WA CHUO CHA MKWAWA WAGOMA MCHANA HUU WAKIDAI HELA YA KUJIKIMU
JAMII 3:18 AM
WANAFUNZI wa mwaka wa pili na watatu katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa Iringa leo wamegoma kuingia madarasani wakishinikiza bodi ya mikopo kuwapa fedha zao za chakula na malazi kiasi cha zaidi ya shilingi 600,000.
Wanafunzi hao walianza mgomo huo majira ya asubuhi na kudumu kwa zaidi ya masaa matano huku uongozi wa chuo hicho ukiwataka wanafunzi hao kuingia madarasani kuendelea na masomo .
Wakizungumza na MPEKUZI wetu kwa sharti la kutotajwa majina yao ,wanafunzi hao walisema kuwa wanashindwa kujua sababu za msingi za bodi ya mikopo kushindwa kuwapa fedha hizo huku vyuo vingine wakiwa wameingiziwa fedha hizo.
Kuwa uongozi wa chuo hicho umewataka wanafunzi hao kukamilisha kujaza fomu za kujisajili kwanza ndipo washughulike na madai hayo jambo ambalo wamedai kwao ni vigumu kufanya hivyo.
Hata hivyo walisema kuwa wapo tayari kuendelea na mgomo huo iwapo badi ya mikopo itashindwa kuwatimizia madai yao na kuwa kwa sasa wanalazimika kushinda bila kula kutokana na kukosa fedha za matumizi.
Wanafunzi hao walisema kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 650,000 wanazodai kiasi cha shilingi 450,000 ni fedha kwa ajili ya chakula na malazi na kiasi cha shilingi 200,000 ni fedha za stationary .
Uongozi wa chuo hicho na ule wa serikali ya wanafunzi haukuwa tayari kuzungumzia sakata hilo