WANAUME WABUNI MBINU MPYA ZA KUWANASA WAREMBO JUKWAANI


Siri nzito imevuja kuwa VIGOGO wa mjini ‘mapedeshee’ wanaotimba kwenye kumbi za starehe na kuwatuza wanenguaji wa bendi mbalimbali Bongo, wamebuni mbinu mpya ya kuwanasa warembo hao kwa kuwapa noti zilizoandikwa namba zao za simu

Uchunguzi  umebaini kuwa mbali na noti hizo kuandikwa namba simu, pia huchorwa jina la pedeshee husika.
Wakizungumzia ishu hiyo, baadhi ya wakatanyonga  katika bendi zinazotamba Bongo walikuwa na haya ya kusema:

BEATRICE JOHNSON ‘BABY TALL’ WA TWANGA: “Siwezi kuwasemea wenzangu lakini ni kweli huwa wanatumia mtindo huo wa kugawa namba za simu. Siyo hapa Bongo tu, hata Uarabuni kuna mchezo huo.”

ASHA SAID ‘SHARAPOVA’ WA TWANGA: “Pesa zote ninazotuzwa mimi huwa nampatia mpenzi wangu kabla hatujaanza kuzitumia, kwa hiyo wanapoweka namba za simu ni kama wanajisumbua kwa sababu mtumiaji wa kwanza anakuwa ni ‘maiswiti’ wangu.”

SUZANE CHUBWA ‘QUEEN SUZY’ WA FM ACADEMIA: “Siyo namba tu, huwa wanatupatia hata ‘business cards’ wakiambatanisha na fedha zao wakidhani tutawatafuta.”

OTILIA BONIFACE WA EXTRA BONGO: “Wengine huwa wanajifanya wanatuza halafu wanatupatia vikaratasi vyenye namba za simu.”

Posted by Bigie on 7:15 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.