AUNT EZEKIEL ATANGAZA KUJITOA KATIKA KLABU YA "BONGO MOVIES"


Aunt Ezekiel ametangaza kujitoa rasmi katika klabu ya wasanii ya Bongo Movie yenye makazi yake Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.

Akizungumza na Mpekuzi wetu hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Aunt alisema amechukua uamuzi huo kwa lengo la kujiepusha na wabaya wake.

“Sioni sababu ya kuendelea kukaa katika kikundi au chama ambacho ndani yake kuna wabaya wangu, mwisho kunaweza kutokea kitu kikubwa nikaonekana kituko ndani ya jamii. Sitaki hilo litokee, ndiyo maana nimeamua kujitoa,” alisema Aunt.

Alisema, licha ya kuwa na bifu la wazi na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, wapo wengine ambao hawaangaliani kwa jicho zuri, ndiyo maana akaona kujiondoa ni bora zaidi kwake.

Alimalizia: “Nitabaki kuwa msanii wa kawaida. Sitaki kujihusisha na kitu chochote kuhusu Bongo Movie, huo ndiyo msimamo wangu.”

Posted by Bigie on 7:09 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.