"MAISHA YAMEKUWA MAGUMU KULIKO NILIVYOKUWA NIKIFIKIRIA"... IRENE UWOYA
JAMII 6:40 PM
BAADA ya misukosuko ya ndoa yake, Irene Pancras Uwoya , amekiri kuwa sasa maisha ni magumu kuliko alivyokuwa akiyafikiria.
Akizungumza na mpekuzi wetu jijini Dar es Salaam juzikati, Irene aliweka wazi kuwa hajawahi kupitia maisha ya ukata kama anayokumbana nayo hivyo ameanza kuwa makini katika matumizi ya kile anachopata.
“Asikwambie mtu, nimeonja joto ya jiwe, nimeamua kupunguza matumizi yote yasiyo ya lazima ili angalau niende sawa na maisha haya,” alisema Uwoya
Staa huyo aliyetamba vilivyo katika Filamu ya Dj Ben inayosumbua sokoni, amewataka mastaa wenzake kuwa na nidhamu ya fedha kwani zikiondoka zinatoweka moja kwa moja.






