MR.BLUE AANZA MAANDALI YA KUFUNGA NDOA

Baada ya kila mmoja "kuguess" anachokijua kuhusu  mke mtarajiwa wa Staa wa single ya Tilalila  ya  MR BLUE, hatimaye,msanii huyo ameamua kuanika ukweli.

Akiwa katika mahojiano maalumu na mpekuzi wetu ,Blue mwenye umri wa miaka 24, alifunguka na kueleza mengi juu ya mahusiano yake.Kwanza alianza kwa "mbwembwe" za kumnadi mchumba wake kuwa ni STAA kutokana na kile anachokiamini yeye kuwa "mtoto wa nyoka naye ni nyoka"..

“mpenzi wangu mimi ni staa kwa ajili yangu ila ni mtu wa kawaida na Mungu akijalia ndani ya miaka mitano ijayo, nitakua nimeshamaliza swala la ndoa, yani nitakua nimemuoa, sasa hivi ni time ya kutulia, huyu ndio mpenzi wangu niliekaa nae kwa miaka nane mpaka sasa”Alisema Mr.Blue


alipoulizwa na Mpekuzi wetu  kuhusu taarifa za kuwa na mahusiano ya kimapenz na msanii NAJMA ambae aliuza sura kwenye video ya TABASAMU, Mr.Blue alisema :
“hapana yule sio mpenzi wangu, mpenzi wangu anaitwa WAHYDA


Huyu ndio WAHYDA, mke mtarajiwa wa MR. BLUE

Posted by Bigie on 8:10 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.