BIFU LA "AUNT" NA " RAY" LAZIDI KUSHIKA KASI
JAMII 1:01 AM
Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa hao wana mgogoro wa kufa mtu ambapo eti hawasalimiani na hata ukiwaweka pamoja, huwezi kuwaona wakizungumza.
Ilidaiwa kuwa bifu hilo lilianza tangu kipindi kile Klabu ya Bongo Movie ilipotangaza kumfungia Aunt kuigiza na baadaye kumwachia huru, lakini Ray alituhumiwa kushikilia msimamo wake kuwa hatamchezesha kwenye filamu zake.
Ilisemekana kuwa Aunt alipofikishiwa ishu hiyo na wapambe nuksi, alilalama kivyake na kudai hafanyi filamu kwa msaada wa mtu mmoja, hivyo hawezi kupiga goti, kila mtu akachukua hamsini zake.
Baada ya kupata tetesi hizi,mpekuzi wetu alimtafuta Aunt ambaye alikuwa na haya:
“Katika maisha yangu huwa naumizwa sana na mtu anayenizibia riziki bila sababu.
“Nisingependa kuzungumza sana juu ya bifu, lakini ni kweli nina muda mrefu sijasalimiana na Ray.”
Alipotafutwa Ray ili kupata mzani wa habari hiyo, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.






