"SIJAWAHI GOMBANA NA MUME WANGU.....WANAOTUPAKAZIA NI WANAFIKI TU"......JACK PATRICK
JAMII 12:45 AM
SIKU chache baada ya kuwepo kwa uvumi wa kuvunjika kwa ndoa changa ya Jacqueline Patrick na Abdullatif Abdallah Fundikira, wawili hao wamefunguka laivu.
Hivi karibuni habari zilizagaa kuwa wawili hao wameachana kwa ugomvi wa kurushiana ngumi nyumbani wanakoishi Mbezi Beach, Dar es Salaam huku Jack akidaiwa kufunga virago na kutimkia kusikojulikana.
Wakizungumza kwa nyuso za kushangaa ndani ya ofisi za magazeti maarufu hapa nchini (Global publishers) , mwishoni mwa wiki iliyopita, wawili hao walisisitiza kuwa hawajawahi kugombana huku wakitupa mawe kwa wabaya wao wanaotangaza kuvunjika kwa muunganiko wao.
Jack ambaye ni modo ‘high class’ alitambaa na mistari kuwa kuna baadhi ya marafiki zake ambao hawakuamini kama angeolewa na kutulia hivyo wanangoja kwa hamu kubwa kuona ndoa hiyo inasambaratika.
Huku akimkumbatia mumewe ambaye ni mfanyabiashara mkubwa Bongo, alifunguka: “Hatujawahi kugombana, wanaotapakaza ishu hiyo ni wale waliosema siwezi kuolewa, sasa mimi nina nini hadi nisiweze kuolewa? Nina kilema gani? Kiukweli mimi ni ‘wife material’ na ni mke kamili.”
Hata hivyo, wawili hao walikiri kuwa adui namba moja wa ndoa yao anayefanya yote hayo ni jamaa ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Jack.
Jack na Abdullatif walifunga ndoa jijini Dar hivi karibuni ambapo wameshauriwa kufumba macho na kuziba masikio kukwepa maneno ya mashambenga.






