DR. SLAA ATAZAMIWA KUTUA JIJINI MBEYA ALHAMISI YA WIKI HII
JAMII 5:39 AM
Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Dkt.Wilbroad Slaa anatarajia kutua Jijini Mbeya Januari 12 kwa ziara ya kuhamasisha chama mkoani humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa CHADEMA mkoani Mbeya Eddo Makatta, Dkt.Slaa ataingia Jijini Mbeya na kufanya mikutano ya ndani kisha mikutano yahadhara katika maeneo mbalimbali ya wazi.
Makatta alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya mikakati ya chama hicho kukutana na wapigakura wake kwa nia ya ,kuwazindua juu ya mambo mbalimbali ya hujuma na ufisadi dhidi ya wananchi unaofanywa viongozi waliopo madarakani.
Alisema kuwa ziara ya Dkt. Slaa inakuja wakati kukiwa na mijadala na midahalo mbalimbali inayoendelea juu ya marekebisho yaKatiba ya Jamhuri ya Muungano






