MDOMO WAMPONZA NORA .......NDOA YAKE SASA NI "VIPANDE VIPANDE"
JAMII 6:16 PM
Ndoa ya staa wa sanaa za maigizo Bongo, Nuru Nassor ‘Nora’ imeingia dosari kubwa kwa sababu yupo kwenye mgogoro mzito na mume wake, Masoud Ali ‘Luqman’.
Habari kuwa Nora na mumewe Luqman hawaelewani, zinadaiwa chanzo chake ni kauli ya mrembo huyo aliyoitoa hivi karibuni katika baadhi ya vyombo vya habari.
Nora alitoa kauli nzito kuwa yupo tayari kuomba talaka endapo mume wake hatamruhusu kucheza filam.
Mume wake aliposoma gazetini kauli hiyo, moja kwa moja alipitisha uamuzi wa kumuacha mkewe lakini ndugu wameingilia kati kunusuru ndoa hiyo.
Hata hivyo, maelewano bado siyo mazuri. Wamesuluhishwa lakini mwanaume bado haelewi. Anasema Nora amemdhalilisha kupita kiasi na anaamaini hana mapenzi naye.
Jitihada za mpekuzi wetu kumpata Luqman ziligonga ukuta lakini Nora alipopatikana , alikiri kuwepo kwa mtafaruku mzito na mume wake.
“Naumia sana, sikutegemea kama yale maneno yangemuudhi mume wangu na watu wengine, kwa sasa nipo katika hali ngumu ya kuweka mambo sawa ili nieleweke kwamba sikuwa na nia mbaya.






