MENEJA WA TIP TOP CONNECTION AKABILIWA NA TUHUMA ZA UCHAWI
JAMII 2:04 AM
Meneja wa kundi la TIPTOP CONNECTIONS Babtale leo amezungumzia tuhuma zilizoenea kuhusu yeye kwamba ni MCHAWI. Stori ambazo zimeandikwa na mitandao mbalimbali zinaeleza kwamba boss huyo wa Tip top connection ni mchawi na huwa anatembea na kibegi chake fulani ambacho hakiachi kamwe.

kibegi cha Babtale kinachotajwa kuwa na uchawi wake!
Mpekuzi wetu alifanya mazungumzo na Babtale kuhusiana na tuhuma hizi ambapo alisema:
“kuna mambo mengi nafanya mazuri lakini watu hawayaoni, kibegi changu nakitumia kuhifadhi vitu vyangu, kuna laptop na vitu vingine.
Mtu anaponiandika kwamba Tale mchawi amempoteza msanii huyu, amemdidimiza msanii huyu, wanashindwa kuelewa kwamba mwanzo mimi ndiye niliyemfanya huyo msanii anga’e, na akiondoka kuwa chini yangu wengi wanafeli kwa sababu hawana MANAGEMENT nzuri”
“Kuna mambo mengi nafanya lakini hakuna anayesifia, mimi na Said Fela wa TMK family ndio tunaomsimamia DIAMOND sasa hivi, tumemrudisha Ferooz na mchiriku wake, tumemrudisha SUMALEE lakini hakuna anae tusifia.Watanzania hawakusifii mpaka Ufe, sio kitu kizuri”






