FATAKI ANASWA AKIVUNJA AMRI YA SITA NA MWANAFUNZI WA MIAKA 16 AMBAYE YUPO KIDATO CHA PILI










WAKATI serikali na taasisi mbalimbali zikihamasisha kuwalinda wanafunzi kutoka kwenye mikono ya wanaume wanaofanya mapenzi na wanafanzi, ‘mafataki’, Mustafa Kachenga (39), mkazi wa Kiluvya, jijini Dar es Salaam amenaswa gesti (jina tunalo) akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili.

Tukio hilo la aibu ambalo lilishuhudiwa na baadhi ya majirani, lilijiri saa tano asubuhi ya Aprili 16, 2012 ndani ya gesti hiyo maarufu iliyopo Manzese, jijini Dar es Salaam.


Habari zinasema, Kachenga ni dereva wa kigogo mmoja Wizara ya Ujenzi na kwamba, siku ya tukio alimpeleka bosi wake huyo kwenye semina na kumwacha kwa maelekezo ya kumrejea jioni.

SIMU YA MTOA TAARIFA
Ilikuwa wakati waandishi wetu wakiwa katika harakati za kusaka habari, walipigiwa simu na msamaria mwema mmoja mwanaume (hakutaka kujitambulisha jina) akinyetisha kuwa amemuona mwanafunzi mmoja akiwa na sare za shule akizama ndani ya gesti hiyo.

Mtoa habari huyo aliendelea kueleza kuwa mara baada ya mwanafunzi huyo kuingia, akafuatia ‘fataki’ na hivyo kuzua maswali kwa waliowaona kuhusu makutano yao ndani ya gesti hiyo iliyopo uchochoroni.

“Nilipoona wamezama ndani wote, ndipo na mimi nikaenda kuchungulia, nikawaona wakizama chumba namba tano, ndiyo maana nawaita muwahi hapa sasa hivi, wapo,” alisema mtoa habari huyo na kukata simu.

POLISI, MAPAPARAZI WAINGIA KAZINI
Mara baada ya kupata taarifa hizo, timu yetu ya mapaparazi ilifunga safari mpaka Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo na kutoa taarifa ambapo askari watatu wasiokuwa na sare walitolewa kwa ajili ya msafara wa kwenda kumnasa fataki huyo.

Kwa kutumia msaada mkubwa wa chombo hicho cha dola, uongozi wa gesti hiyo ulipewa taarifa, chumba namba tano kikagongwa na kufunguliwa na mwanaume huyo aliyejitupia taulo kama yuko kwake Kiluvya ambapo aliwekwa chini ya ulinzi.

Mwanafunzi huyo anayesoma Sekondari ya Kiluvya, alikutwa akiwa mtupu juu ya kitanda, alishtuka kwa ugeni wa ghafla na kuanguka sakafuni akijifanya amepoteza fahamu ingawa haikuwa kweli.

ETI MWANAUME AJITETEA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanaume huyo aliyekuwa na gari la serikali namba STK alipobanwa kuhusu uwepo wake na mwanafunzi ndani ya gesti hiyo alisema amekuwa akimsaidia kumsomesha hivyo na yeye huwa ‘anasaidiwa mambo f’lani’.

Hata hivyo, jamaa huyo akaapa kuwa hatarudia tena baada ya kuligundua kosa huku, kama kawaida ya binadamu, akimlaumu shetani kuwa ndiye aliyemdanganya.

DENTI KILIO MUDA WOTE
Wakati mpenzi wake huyo akitaitiwa na maswali ya awali, mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 alikuwa akichuruzika machozi muda wote.

SAFARI YA KITUONI
Maafande shupavu waliwatwaa wawili hao ndani ya usafiri wao sanjari na mapaparazi wetu mpaka Kituo cha Polisi cha Magomeni ambako walitoa maelezo na baadaye kuswekwa mahabusu kwa kila mmoja na jinsi yake.

Source:Global Publisher

Posted by Bigie on 12:12 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.