HAYA NDO MAMBO YANAYO JIRI HUKO BUNGENI LEO HII....ENDELEA KUWA NASI


(HAPA ILIKUWA NI MIDA YA ASUBUHI)
Kumekucha baada ya hekaheka za jana huku macho na masikio yakiendelea kutosadiki yanayotarajiwa kujiri hasa baada ya kigugumizi kuwatawala wanaokusudiwa kufunguwa midomo yao kupaza sauti itakayokata mzizi wa fitna na kufungua ukurasa mpya wa historia ya uwajibikaji katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Kwa ujumla wabunge wanaoonekana kuranda hapa katika viwanja vya bunge ni wachache saana, sijui wengine wako wapi na ORDER PAPER haionyeshi kama PM kapangiwa kusema jambo licha ya kuwa yeye a kama mtendaji mkuu wa serikali hawajibiki kufanya hivyo kwani wakati wowote anaohitaji kutoa taarifa kwa maelekezo na mwasiliano na Spika anaweza kufanya hivyo.

Tafakuri ni zito, na muda punde Bunge litaanza.

Upande anaopitia waziri mkuu  ulinzi upo kuashiria anakuja na muda wowote atafika hapa mjengoni

******************************************************
UPDATES: HOFU YANGU YA KUTOWAONA WABUNGE ILIKUWA SAHIHI.( ilikuwa majira ya saa  tano)
  Waziri mkuu ana mjadala Mkali tena, Sitashangaa Maamuzi haya yakachakachuliwa Vibaya na zikazuka Hadithi mpya kabisa ambazo zitasononesha Vibaya mioyo ya Watanzania waliokwishajawa na dukuduku la kujua hatima ya Mawaziri wanaotuhumiwa kwa kutafuna mali ya UMMA na kukosa uwajibikaji.
Tunasaka DETAILS ZAIDI
 
*******************************************************
UPDATES: (SAA SITA NA DK 13)
Muongozo Ulioombwa ni kutaka Ufafanuzi wa Serikali kwa nini haijatoa Tamko lolote wakati Nchi ipo katika sintofahamu zito na wananchi hawajui hatima ya Mawaziri wanaodaiwa  Kujiuzuru. Naomba Muongozo wako Mh. Spika
*******************************************************
 
RECENTLY : PM AMEINGIA MJENGONI NA LOTS OF KABRASHA....Ngoja Tuone

VIDEO:


****************************************************

Spika  amemwita Mnyika JAMBAZI. Kamwambia mbowe "ulikuwa umepitwa ila shukuru muongozo wa huyu JAMBAZI wako (Mnyika) umekuokoa"


*************************************************** 
MHE. SPIKA KAMWOMBA RADHI MH. MNYIKA KWA NENO 'JAMBAZI', LISOMEKE "JAMAA"

 ******************************************************
UPDATE: MEDIA zimetega anapotokea PM kwa shauku ya aina yake, ataingia mitini kamajana au atatoa neno?????
******************************************************

Posted by Bigie on 2:43 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.