UPDATE TOKA ARUSHA: VIJANA WATANO WANYONGWA KIKATILI JIJINI ARUSHA
JAMII 2:31 AM
Habari za kusikitisha kutoka Jijini Arusha leo Jumamosi April 21, 2012 zinaeleza kuwa jumla miili ya watu watano imepatikana mapema alfajiri katika Mto Nduruma uliopo maeneo ya Tengeru, baada ya kunyongwa na watu wasiojulikana hadi kufa.
Miili hiyo ya marehemu hao vijana, imekutwa na majeraha kichwani na alama za minyororo shingoni na wengine kamba za katani kama inavyoonekana pichani, hali inayoashiria walifikwa na mauti baada purukushani za kuwanyonga kufanikiwa.
Tayari mmoja amekwishatambuliwa na ndugu zake na kwamba ni kijana wa Sombetini, mjini hapa.
Haijaweza kufahamika sababu hasa za kuyongwa kwao hadi kufa. Miili yote ipo katika hospitali ya Mt Meru kwa utambuzi
BLOG HII INAOMBA RADHI KAMA UTAKUWA UMEKWAZIKA NA PICHA HII





