HII NDO HALI HALISI YA KISIASA NCHINI TANZANIA....MPAKA SASA WABUNGE 75 WAMEKWISHA SAINI KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU
JAMII 12:06 AM

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akisaini karatasi inayokusanya saini za wabunge za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa lengo la kuwasilisha kwa Spika mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Zitto Kabwe.
MKAKATI wa kukusanya majina 70 ya wabunge kama sehemu ya kukamilisha utaratibu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, umepamba moto na hadi kufikia jana jioni, wabunge 75 walikuwa wameunga mkono hatua hiyo, watano kati yao wakitokea chama tawala CCM.
Endapo mchakato huo utakamilika, Pinda atakuwa ameingia katika historia ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na Bunge, tangu Tanzania ipate uhuru wake Desemba 9, 1961





