KWAYA YA CCM MAGU NAYO YAHAMIA CHADEMA

 
Kwaya ijulikanayo kama Kwaya ya  Ng'ombe ya Magu Mjini Mkoani Mwanza yenye watu 45 imejiengua CCM na kuhamia CHADEMA jana jioni. Wanakwaya hao wamepokelewa jioni na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Magu ndugu  Katinde aliyeongozana na Katibu wa CHADEMA Jimbo la Magu mjini Bahati Simon.

Hii ilikuwa ni Kwaya  waliyoitumia sana kwenye kampeni na kwenye kila matukio yao na vifaa vyao vyote vya muziki vilitunzwa kwenye ofisi za CCM wilaya ya Magu. siku mbili kabla ya kuhamia CHADEMA walitafuta kambi ya muda na wakatunga nyimbo za kumsifia Dr. Slaa ambaye atafanya ziara hivi karibuni wilayani Magu.
 
Na Samson Mwigamba

Posted by Bigie on 1:59 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.