FUMANIZI LA MR. NICE
JAMII 2:58 AM

MWANAMUZIKI aliyevuma miaka ya nyuma kunako anga la Bongo Fleva, Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ Jumapili iliyopita kwenye Viwanja vya Leaders Club, Dar wakati Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ilipokuwa ikitoa burudani alinaswa chobingo akiwa na demu.
Awali, Nice alionekana kutumia kilevi huku akijiachia na binti huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja. Alipogundua paparazi anawafuatilia hatua kwa hatua, staa huyo alihama eneo hilo na kwenda sehemu iliyokuwa na giza kuendelea na starehe zake.
Katika pitapita ya paparazi wetu, alimkuta Mr Nice na binti huyo akamfotoa picha kadhaa ambapo Mr Nice alipoona mwanga wa kamera alijiziba uso ili kuficha sura yake na kusema:
“Baby twende zetu Billicanas nikazindue wimbo wangu mpya hapa tayari kimeshanuka.”





