SHUGHULI MBALIMBALI ZA RAIS KIKWETE AKIWA MJINI ADDIS ABABA,ETHIOPIA
JAMII 1:58 AM

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mdahalo wakati wa Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika, akiwa na viongozi wengine wa nchi mbalimbali waliohudhuria.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa,Bw. Koffi Annan walipokutana katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bishara la Kimataifa - World Trade Organisation (WTO)- Bw Paschal Lamy walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Canada Bi. Berly Oda walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika






