WATEULE WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI
habari za kitaifa, siasa 8:08 PM
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda amefunga rasmi semina elekezi ya siku mbili kwa wabunge wapya wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki na kuwataka wabunge hao wakazingatie maslahi ya Taifa katika Bunge hilo. Pichani Mhe. makinda akisisitiza jambo wakati wa hotuba yake ya kufunga semina hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi hadidu za rejea Mwenyekiti wa wabunge wapya wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Adam Kimbisa mara baada ya kufunga rasmi semina hiyo jana jijini Dar es salaam. Picha na Owen Mwandumbya.
