KWA NINI NI MUHIMU KWA WASANII WA TANZANIA KUJIUNGA NA TWITTER


Tangu kuanzishwa kwa ulimwengu wa mitandao ya kijamii, mambo mengi yamerahisishwa zaidi. Mitandao hiyo husasan Facebook na Twitter imeongeza mawasiliano baina ya watu wanaofahamiana, kujenga urafiki, uchumba na mawasiliano kati ya makampuni na wateja yamekuwa rahisi zaidi.

Kwa Tanzania hata hivyo, Facebook ndio mtandao maarufu zaidi kuliko Twitter. Pamoja na urahisi huo wa Facebook bado kuna wasanii wengi ambao roho zao ni ngumu kujiunga kutokana na kutojua faida zake. Kwa upande wa Twitter ambayo wengi hushindwa kuielewa vizuri, siku za hivi karibuni imetokea kutumiwa zaidi na makampuni na watu maarufu kuliko Facebook.

Wasanii wengi wachanga na waliofanikiwa wameshindwa kuitumia fursa ya mtandao huu muhimu katika kujitangaza na kuwa karibu na wadau, hali inayowafanya wazikose fursa nyingi.

Post za Twitter hasa zile zilizoandikwa na msanii mwenyewe kwa mkono wake huwakilisha kauli yake mwenyewe inayoenda kwa mashabiki wake. Sio lazima tena kusubiri interview ya radio ili awaambie albam yake ipo sokoni tayar au kutoa habari sake zozote zinazomhusu msanii mwenyewe.

Fareed Kubanda aka Fid Q ameanzisha utaratibu wa kila weekend kuwapa nafasi watu wanaomfollow ili wamuulize maswali na yeye hujibu yote. Kitu hiki kimempa umaarufu kwenye mtandao huo huku wengi wakijua masuala mbalimbali yanayomhusu na si mpaka kusubiri ahojiwe na radio. Mashabiki wana uwezo wa kumuuliza maswali ambayo hayaulizwi na watangazaji kwenye interview.

Kutokana na ukweli huo, Twitter ni mtandao usioepukika kwa wasanii ama bendi wanaotaka kuongeza nafasi za kuwa wanamuziki wenye mafakinio kwenye biashara ya muziki.


Mwenyekiti mtendaji wa mtandao wa Headliner.fm (mtandao mahsusi wa marketing kwa wanamuziki) Mike More anasema Twitter ni ‘njia iliyonyooka kuelekea kwa mashabiki.’

Faida kubwa na ya wazi ya wasanii kutumia Twitter ni uwezo wake wa kutoa mawasiliano ya moja kwa moja na mashabiki. Twitter imewasaidia sana wasanii kama AY na Diamond miongoni mwa wengine waliojiunga, kuongeza idadi yamashabiki nje ya Tanzania. 

Wasanii wengine wamepata show nyingi za nje kupitia Twitter. Uzoefu unaonesha pia kuwa wasanii wengi wako active zaidi Twitter kuliko Facebook kutokana na mitandao hiyo kutofautiana mfumo na aina ya watumiaji. Msanii aliyepo Facebook pekee hukosa fursa ya kubadilishana mawazo na wasanii wengine kwakuwa wao hutumia muda mwingi Twitter.

Ni rahisi sana kwa msanii mchanga kujitangaza Twitter hasa pale anapotumia mgongo wa msanii mkubwa. Kwa mfano msanii mchanga anaweza kutweet kitu ambacho kikimpendeza msanii kama AY mwenye followers takriban 15,000, anaweza kukiretweet na kikasomwa na watu wote wanaomfuata ambao watamtambua msanii huyu huku wengine wakiamua kumfollow. Hili huwezi kulipata Facebook.


Ukishajiunga na Twitter msanii unapaswa kuzingatia yafuatayo:

Kuwa mhudhuriaji.
Ukishaingia Twitter, unahitaji kuanza kutweet. Kama mitandao mingine ya kijamii, utaielewa kwa haraka kama ukiwa mtumiaji mzuri. 

Ukishafungua profile ya Twitter unatakiwa kuamua kama utakuwa ukitweet kama msanii ama member wa kundi/bendi fulani. Ni wazi kama wewe ni solo artist chaguo hili ni kwajili yako na rahisi zaidi kukuunganisha na mashabiki.

Hata hivyo inapendekezwa kuwa kama utafungua akaunti ya bendi tweet zenu zioneshe ‘ninyi’ mmesema jambo ama kama ni mmoja akiandika basi ataje jina lake pale inapotakiwa.
Hakikisha tu kuwa mtu atakayewajibika kusimimamia akaunti awe anayeweza kujichanganya, mcheshi, funny n.k.

Andika historia yako
Sehemu ya kuandika historia yako umepewa meneno machache sana hivyo yatumie vizuri kuandika maneno yatakayorahisha wewe upatikane kirahisi kwenye search engines (Search Engine Optimisation). Hivyo unatakiwa kuelezea kwa makini unachofanya na muziki wako kwa maneno yatakayowasaidia watu kukupata kirahisi kama wakiserch jina lako kwenye Google.

Anza kufollow
Wafuate marafiki zako kwanza, watu wanaokuvutia, watangazaji, madj, radio na watu wengine wote wanaokuvutia. Epuka kasumba kuwa wewe ni supastaa hivyo hutakiwi kufollow watu.

Utweet kwa kiasi gani?
Mara kwa mara ni vizuri zaidi. Tweet moja kwa siku ni bora kuliko tweets tano kwa siku halafu unakaa mwezi mzima.
Jaribu kufikiria kama vile upo kijiweni mkiongea na washkaji.
Ni ngumu kujua kama unazidisha. Kama unahisi unazungumzia kila tukio unalofanya na watu wanaokufuata hawaoneshi kujibu basi hapo huenda umepitiliza. Mfano “Nimekula ugali na nimeshiba sasa nataka kulala” Unadhani tweet hii itavutia majibu?

Jichanganye kwenye mazungumzo ya wengine
Sio lazima iwe kuhusu wewe tu. Ni kuhusu wao pia na mazungumzo unayofanya nao. Hiyo ndio kazi ya alama ya ‘@’. Pale mtu anapotaka kuchangia kitu ulichotweet atatumia alama hiyo. 

Hii ni nzuri kwakuwa watu wataona umejibiwa. Na mtu ambaye hajakufollow anaweza kuvutiwa kufanya hivyo ili akujue zaidi.
Unaposhiriki kwenye mijadala mbalimbali inakufanya uongeze uhusiano na mashabiki na kujipatia wengine zaidi.
Kwa upande mwingine unaporukia jambo ulilovutiwa nalo kwa mtu unayemfollow na kuchangia mada ama mazungumzo yake inakupa credit zaidi.

Hivyo ndivyo watu watu wanataka kuona sio zile tweet za “Angalia website yangu blah blah blah”

Hata hivyo usipitilize ku‘@reply’. Kama umejikuta umeingilia mazungumzo ya watu na ukaona majibu unayopata ni ya aina hii: (‘I agree’ / ‘That’s funny’, Lmao ama LOL) basi jua umezidisha. Hii inakufanya uonekane unajipendekeza, uko shallow na kiwango cha kelele na kurukia mazungumzo ya wengine kwa watu wanaokufuata kitasababisha wakuunfollow.

Sambaza masuala muhimu
Hii ni njia nzuri sana kuitumia kwenye Twitter. Unaweza kuwa unaweka link ya website ama radio ya online inayocheza nyimbo zako na vitu ambavyo vinakuvutia na wale wanaokufollow wanavipenda pia.

Retweet
Kutweet tena kile alichotweet mtu baada ya kukipenda ni kitu cha msingi kwenye mtandao huu.

Hii itawafanya watu wakufollow zaidi na kuamini kuwa unataka kusambaza mambo mazuri na si kupromote muziki wako pekee.

Tweets za watu ambao unaweza kuzire-tweet zinaweza kuwa za wasanii wenzako kupromote show zao, uzinduzi wa albam nk! share the love!

Faida yake ni kuwa wale ambao utakuwa unaretweet mambo yao watalipa fadhila pia kwa kufanya hivyo pale utakapokuwa unapromote kitu chako.

Hata hivyo usiretweet kila linalosemwa. Hii itakufanya uonekane mtu usiyeweza kupembua mambo.
Usisahau lakini kuwa mtu anaporetweet jambo lako tena kwa wafuasi wengi kuliko ulionao wewe, anapaswa kuambiwa ‘Asante.’

Direct Message
DM mara nyingi hutumiwa vibaya na inaweza kukuletea shida.

Inaweza kuwa njia nzuri kwa mazungumzo ya faragha lakini unapaswa kuwa makini nayo.

Mwisho kama msanii bado hujajiunga na Twitter fahamu kuwa unapitwa na mengi na fanya haraka kujiunga kabla hujachelewa.

Posted by Bigie on 1:21 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.