SISTER P ATUNDIKWA MIMBA......
6:24 PM
Rapper wa kike aliyewahi kutamba nchini na ngoma kadhaa ukiwemo‘Anakuja’, Sister P anadaiwa kuwa mjamzito, kwa mujibu wa mtu aliye karibu naye.
Msanii wa kizazi kipya, Tanzanite ndiye aliyeitoa habari hiyo kupitia Facebook kwa kuandika, “hatimae SISTER P apigwa mimba daaaaah, nangoja kuitwa anko daaah siamini.”
Tumeamua kumpigia simu Tanzanite ili kuthibitisha habari hizo ambaye alisema ni kweli kwakuwa Sister P ni kama dada yake na wapo karibu sana.
Tanzanite amesema ujauzito wa Sister P bado ni mchanga lakini amekuwa akionesha dalili zote kuwa ni mjamzito.
Kama ni habari hizo ni za kweli basi hongera kwake Sister P.






