WASANII 10 CHIPUKIZI AMBAO WAMEFANYA VIZURI MWAKA 2012
BONGO FLEVA, habari za kitaifa 6:30 PM
Zikiwa zimebaki siku chache tu mpaka tuumalize mwaka 2012,Mtandao huu umewaangalia wasanii 10 wapya wa Tanzania ambao wamefanya vizuri mwaka huu wa 2012. Hii ndio list ya wasanii hao.
1. Ally Nipishe
Ally kwenye picha hapo juu ni kijana aliyeupendezesha wimbo wa Mwasiti, ‘Mapito’, ambao ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri zaidi mwaka 2012.
Kijana huyu kutoka THT, ni tishio kubwa kwa wasanii wenye uimbaji kama yeye ambao ni pamoja na Barnaba, Amini na wengine. Kwa sasa ana wimbo wake mwenyewe uitwao My.
2. Vanessa Mdee

Mtangazaji huyu wa MTV Base na Choice FM ameonesha uwezo mkubwa katika kuimba mwaka huu baada ya kushirikishwa kwenye wimbo Money wa AY na Me and You alioshirikishwa na Ommy Dimpoz.
Me and You unafanya vizuri kwenye radio za Afrika Mashariki na ndio uliodhihirisha uwezo mkubwa wa uimbaji aliojaaliwa mrembo huyu.
Hivi karibuni, Vanessa ameonesha uwezo mwingine wa kurap katika wimbo alioshirikishwa na Dj Choka, Press Play. Watu wengi wanausubiri ujio wake mwenyewe.
3. Walter Chilambo

Mshindi huyu wa kitita cha shilingi milioni 50 za Bongo Star Search 2012 mwenye mashabiki lukuki nchini ameonesha kila dalili ya kuiondoa aibu ya washindi waliopita wa shindano hilo ambao wameshindwa kufanya vizuri sokoni. Sauti ya pekee aliyonayo Walter inaashiria kuwa mwaka 2013 utakuwa wake pia.
4. Mirror
Mirror (Kulia)5. Cliff Mitindo

Cliff ni rapper mwenye uwezo mkubwa wa Freestyle.
Alifanya vizuri kwenye cypher ya Fiesta 2012 iliyowakutanisha mastaa kibao wakiwemo Godzilla, Fid Q, Babuu wa Kitaa, Nikki wa Pili, Stamina na wengine. Ana ngoma yake mpya iitwayo Ha ha ha ambayo inafanya vizuri redioni na kuuonesha upekee wake katika uandikaji na uwasilishaji wa michano.
6. M-Rap
M-Rap (kulia) akiwa na Pancho7. Kankaraga

Hili ni kundi la wasanii watatu wa kike kutoka THT. Akina dada hawa utawapenda ukiwaona kwenye stage wakiperform.
Wakiwa na kila sifa za kuwa madansa, Kankaraga wamedhihirisha uwezo mwingine mkubwa wa kuimba hasa kama ukisikiliza wimbo wao wa kwanza, ‘Kankaraga’. Mwaka 2013 bila shaka umewawekea nafasi yao.
8. Young Killa
Young Killa aliyevua shatiYoung Killa alikuwa miongoni mwa washindi wa Super Nyota ya Fiesta na alifanikiwa kuzunguka mikoa yote Fiesta ilikofanyika mwaka huu. Uandishi wa nyimbo zake una uelekeo wa wasanii kama One The Incredible, Nikki Mbishi na Stereo.
9. Vida

Kama umewahi kuusikia wimbo uitwao ‘Baba Awena’ utakuwa umemsikia dada mmoja mwenye sauti tamu iwezayo kumtoa nyoka pangoni. Huyo ni Vida zao jingine kutoka TH. Katika wimbo huo Vida amemshirikisha Linex.
10. Kadgo
Kadgo (kushoto) akiwa na Fid







