AIBU ZA WASANII: MATITI YA BABY MADAHA YAANIKWA NJE KAMA NYANYA




STAA  wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amejikuta akiumbuka mbele ya mashabiki wake baada ya matiti a.k.a nido zake kuchomoza na kuonekana hadharani akiwa jukwaani na kusababisha midume yenye ukame kumzengea.


Tukio hilo la aibu isiyo na kipimo lilishuhudiwa na mwanahabari wetu usiku wa kuamkia Septemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako kulikuwa na tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2012.

Baby Madaha alifanya kioja hicho baada ya kutakiwa kupanda jukwaani kuimba na Juma Kassim ‘Nature’ ambaye wameshirikiana katika moja ya nyimbo zake.

Bila hiyana, Baby alipanda stejini kwa mbwembwe na kujikuta akimwaga radhi  kwa kuonesha matiti hadharani na kusababisha umati uliokuwa umefurika uwanjani hapo kulipuka kwa shangwe huku mwanadada huyo akiendeleza libeneke la shoo kali.


Baada ya kushuka jukwaani ndipo dada huyo alipovamiwa na wanaume wakware ambao walimbonyeza Kizenji hadi alipookolewa na mabaunsa na kupelekwa nyuma ya jukwaa.

Posted by Bigie on 1:36 AM. Filed under , , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.